
WAZIRI WA KILIMO UMWAGILIAJI MALIASILI NA MIFUGO MH: SHAMATA SHAAME KHAMIS AMEZINDUA KAMPENI ZA KUDHIBITI NZI WA MATUNDAPosted: 2022-07-04
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis amezindua Mradi wa kampeni ya kudhibiti nzi wa matunda uliyofanyika Kitope Zanzibar. Amesema Zanzibar ina fursa kubwa ya uzalishaji wa matunda na mboga, ambayo ni chanzo cha upatikanaji wa kipato Kwa wakulima wadogo wadogo, hata hivyo uvamizi wa nzi wa matunda umekua changamoto kwa uzalishaji na ubora wa mazao Kama vile embe, mapapai na mabungo. Nzi waharibifu wa matunda ambao wamejitokeza Zanzibar mnamo mwaka 2004, ni hatari sana ambao husababisha hasara kwa wakulima hadi kufikia asilimia 80 na hupelekea biashara ya matunda hususan embe kwenda nchi za nje kuzuiliwa. Amewataka wakulima kuthamini juhudi za Serikali Kwani Kwa makusudi mazima imeamua kuanzisha Mradi wa kudhibiti nzi wa matunda kwa lengo la kuongeza uzalishaji na uhakika wa chakula, tija na hatimaye pato la taifa. Mradi huu wa miaka minne na utatekelezwa katika Shehia zote za Unguja na Pemba.