
WAZIRI WA KILIMO UMWAGILIAJI MALIASILI NA MIFUGO MHE. SHAMATA SHAAME KHAMIS AWATAKA WAFANYAKAZI WA MSITU WA MAUMBILE MASINGINI KUWAJIBIKA KATIKA MAJUKUMU YAOPosted: 2022-07-04
Viongozi na Wafanyakazi wa Idara Misitu wanaofanya kazi katika Msitu wa Hifadhi ya Maumbile Masingini wametakiwa kuwajibika katika majukumu yao ya kazi kuhakikisha wanahakikisha msitu unakua salama na katika hali nzuri. Wito huo umetolewa na Waziri wa kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Hifadhi hiyo. Mheshimiwa Shamata amesema kuwa kuna taarifa za baadhi ya wafanyakazi wanashiriki katika vitendo vya kuhujumu msitu huo. Amewakumbusha kuwa Msitu wa Masingini una umuhimu mkubwa kutokana na kiwango kikubwa cha Hifadhi ya maji iliopo katika msitu huo. Amesema ili kufanikiwa katika majukumu yetu lazima tuwe na mashirikiano baina ya wafanyakazi na viongozi jambo ambalo litaleta umoja. Ametoa maagizo ya kukarabatiwa na kurudisha huduma katika mkahawa uliopo ndani ya msitu huo ili wageni watakaotembelea hapo kupata huduma.