
WAZIRI WA KILIMO MHE. SHAMATA AKABIDHI BASKELI KWA VIONGOZI WA VIKUNDI VYA KUKOPA NA KUWEKAPosted: 2022-06-25
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe Shamata Shaame Khamis amekabidhi baskeli 30 pamoja na visanduki 30 kwa baadhi ya viongozi wa vikundi vya kuweka na kukopa kutoka Shehia mbali mbali vinavyojishuhulisha na kilimo na ufugaji. Vitendea kazi hivyo vimetolewa kupitia mradi wa viungo uliochini ya usimamizi wa Agri-Connect vyenye thamani ya shilingi milioni Saba na laki tano 7,500,000. Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo hapo Maruhubi