
WAZIRI WA KILIMO, UMWAGILIAJI, MALIASILI NA MIFUGO MHE. SHAMATA SHAAME KHAMIS AMEFANYA ZIARA KATIKA TAASISI ZA WIZARA. Posted: 2022-05-18
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo amefanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar (ZARI) iliyopo Kizimbani pamoja na kujionea utafiti wa mihogo mbegu ya kizimbani, katika ziara hiyo Mhe. Shamata aliwataka wataalam wa utafiti wa kilimo kuendeleza utafiti kwani unaleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Wanzibar. Wakati huo huo Mhe. Waziri alipata pia fursa ya kutembelea Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Zanzibar (ZALIRI) iliyopo Kizimbani na kupata maelezo juu ya uoteshaji wa chakula cha ngombe.
Aidha, Mhe. Waziri alitembelea ujenzi wa ghala linalojengwa na mradi wa TANIPAC huko kizimbani wilaya ya magharibi ‘A’ na kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo kutokana na kuchelewa kwa mradi huo. Mhe. Shamata aliwataka wakandarasi wa mradi kuhakikisha wanaendana muda uliopangwa katika kukamilisha ujenzi.