
WAZIRI WA KILIMO, UMWAGILIAJI, MALIASILI NA MIFUGO AKUTANA NA WADAU WA KILIMO HAI - MILELE FOUNDATIONPosted: 2022-05-17
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis amekutana na wadau wa kilimo hai Milele Foundation katika kujadiliana juu ya kuendeleza pamoja na kumaliza mpango kazi wa kilimo hai hapa Zanzibar.
Aidha, Mheshimiwa Shamata aliwataka Milele Foundation kuendeleza mpango kazi huo ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na kuwa tegemezi wa wananchi wa Zanzibar. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za Milele Foundation huko Mweni nje kidogo na Mji wa Zanzibar.