KAMPENI YA KUPANDA MITI KITAIFA 13/04/2019-April 2019

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi imelenga kuotesha jumla ya miche ya minazi 200000 kila mwaka ambayo watapewa wananchi kwa utaratibu maalum bila ya malipo ili kuweza kulirudisha zao la nazi katika hali yake ya awali. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Dkt Makame Ali Ussi wakati alipokua akizungumza na wandishi wa habari huko maruhubi kuhusiana na siku ya upandaji miti kitaifa ambapo mkazo zaidi umewekwa katika kuliimarisha na kulikuza zao la nazi. Amefahamisha kua ingawa kwa msimu huu serikali imeweka mkazo zaid katika upandaji wa minazi hapa nchin i lakini wananchi watatakiwa kuipanda na kuitunza miche hiyo ili Zanzibar iweze kuongeza uzalishaji wa zao la nazi katika kipindi kifupi kijacho. Amefahamisha kua hakuna asiyefahamu umuhimu wa zao la nazi kwa maisha ya uchumi wa nchi hapa Zanzibar lakini kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugona Uvuvi imeweona ipo haja ya kuanzisha kampeni hiyo kwa lengo la kulirudisha zao hilo na kuweza kuzalisha kwa wingi ili kuondokana a na uagizaji wa nazi kutoka nje ya nchi. Dkt Makame amesisitiza haja kwa wananchi kuweza kuitunza na kuihifadhi miti yote iliopo hapa nchini ilkuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabiia nchi ambayo yamekua yakitokezea kutokana uharibifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi wa ukataji wa miti ovyo na kuharibu mazingira ya nchi. Amesema kua miti husaidia kwa kiasi kikubwa kuhifadhi ardhi udongo vyanzo vya maji chemchem mito pamoja naupatikanaji wa mvua ambavyoni muhimu kwa kilimo na ustawi wa maisha yetu ambapo miti pia inahitaji kuishi kama viumbe wengine . Amesema kua ni jambo la kusikitisha kuona kuwa Zanzibar hivi sasa inaagiza nazi kutoka nje ya Visiwa hivi badala ya kuwa wasafirishaji wa zao hilo kama ilivyokua hapo nyuma amabpo hali hii ni ya hatari zaidi na upungufu huu unaonekana zaidi unapofika mwezi mtukufu wa ramadhani hivyo kwa sasa Serikali kupitia Wizara ya Wilimo itasimamia kwa juhudi zote ili kuona kua uhalisia wa zao hilo unarudi kama ilivyoka hapo zamani. Amefahamisha kua wizara ya kilimo imetayarisha Programu ya Uendelezaji wa Zao la Nazi hapa nchini[Zanzibar Development Program 2018-2028]ambapo Programu hiyo ni ya miaka kumi ambayo itaelekezwa kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano katika mikoa yote mitano ya Zanzibar ambapo malengo makuu ya programu hiyo ni kuwahamasisha wakulima kupanda mbegu bora za kiasili za minazi kama vile minazi mirefu na kitamli. Aidha ametoa wito kwa wananchi kuchana na tabia ya kuharibu miti kwa faida ya yetu sote sambamaba na kuwaonya kua hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yoyote atakakamatwa anafanya uharibifu katika misitu ya asili. Kampeni ya upandaji miti kitaifa inategemewa kuafanyika tarehe 13 April 2019 ambapo kampeni hiyo itakua ya kushajihisha uimarishaji na uendelezaji wa zao la nazi itazindulilwa rasmi huko Selem Wilaya ya Magharib A kwa upandaji wa miche ya minazi katika shamba la Serikali Selem ambapo mgeni rasmi atakua Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Makamo wa Pili wa Rais. Kauli mbiu ni Tupande na Tuitunze Minazi Kwa Maendeleo ya Viwanda.