NAIBU WAZIRI AFUNGUA MAFUNZO-February 2019

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MALIASILI MIFUGO NA UVUVI MHE DR. MAKAME ALI USSI AKIFUNGUWA MAFUNZO YA UFUGAJI WA SAMAKI, KAA NA MAJONGOO YALIYOFANYIKA KATIKA KITUO CHA KUTOTOLEA VIFARANGA VYA SAMAKI KILICHOPO BEIT-RAS MKOA MJINI MAGHARIB UNGUJA. AMESEMA SEREKALI INAFANYA KILA JITIHADA KUKUZA UZALISHAJI WA MAZAO YA BAHARI IKIWEMO KUTOA MAFUNZO YA UFUGAJI WA KITAALAM AMBAYO YANAHITAJIKA NA KUFANYIWA KAZI IPASANYO ILI KUWEZA KUPATA MAVUNO MAZURI YATAKAYO MUONGEZEA MFUGAJI KIPATO CHAKE. MAFUNZO HAYO YA SIKU TATU YAMEFADHILIWA NA SHIRIKA LA CHAKULA NA KILIMO (FAO) YALIOWASHIRIKISHA MAAFISA WA UVUVI NA WAFANYAKAZI WA KITUO CHA KUTOTOLEA VIFARANGA ZANZIBAR.