Latest News

Upcomming Events

UZINDUZI MPUNGA KIBOKWA-2018-07-04 08:02:35

SIKU YA MISITU DUNIANI-2018-03-22 08:40:43

USARIFU WA ZAO LA VANILA-2018-03-12 08:18:53

SIKU YA MISITU DUNIANI-March 2018

Waziri wa Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Rashid Ali Juma amesema ukataji wa misitu ovyo unaleta adhari katika maisha ya wanaadamu na viumbe vyengine. Alieleza hayo katika kongamano la siku ya misitu duniani liloadhimishwa kwa mara ya kwaza tarehe 21 march 2018 katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la zamani mjini zanzibar. Kongano hilo lina kauli mbiu isemayo: “misitu na miji endelevu: tuhifadhi misitu na miti kwa ustawi wa miji ili tuishi kwa furaha”. Aidha Mhe. Waziri amesema ukataji wa misitu unaongezeka kwa kasi ya kiwango kikubwa zaidi ya kinachostahiki kukatwa kutokana na hali hii upunguaji, uharibifu na ufyekaji wa misitu imefikia asilimia 1.2 kwa mwaka wakati kasi ya upandaji na urejeshaji wa misitu ni asilimia 0.82 kwa mwaka. Pia ameeleza kuwa hii ni biashara mbovu kwani tunakula mtaji wetu tunatakiwa kukata kidogo na tupande sana misitu ili kuepuka madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanaweza kutuletea adhari kubwa.