USARIFU WA ZAO LA VANILA-March 2018

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi nd. Maryam Juma Abdullah amewataka wakulima wa zao la vanila kusarifu vanila zao kitaalamu ili ziweze kuwa na ubora unaotakiwa katika soko la ndani na nje ya nchi. Akitowa mafunzo ya usarifu wa vanila kwa wakulima 25 wa zao la vanila amesema wizara ikishirikiana na wawekezaji kutoka China watatoa mafunzo ya upandaji wa vanila pamoja na usarifu ili liweze kufikia katika daraja linalotakiwa na kuweza kumpatia mkulima tija na kipato kizuri.