WAZIRI WA KILIMO AKABIDHIWA MATREKTA NA KAMPUNI YA MAHINDRA-March 2018

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Rashid Ali Juma katika ghafla ya makabidhiyano ya matrekta 20 yenye thamani ya shilingi bilioni moja milioni mia nne na sabini na sita laki tatu na sitini na tano alfu mia mbili na hamsini (1,476,365,250/-) kutoka kampuni ya Mahendra na new holland yaliyofanyika mbweni katika jengo la Wakala wa serekali wa matrekta na zana za kilimo Zanzibar. Mhe. Rashid amesema matrekta hayo ni miongoni mwa ahadi za Mhe. rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Sheni kwa lengo la kuendeleza kilimo nchini.