NAIBU WAZIRI AKABIDHI VITENDEA KAZI KWA WENYE NASARI BINAFSI-September 2017

Jumla ya miche milioni mbili na laki tano (2,500,000) inatarajiwa kupandwa katika msimu wa kilimo mwaka 2017/18 katika Idara ya misitu na maliasili zisizorejesheka . Akikabidhi vitendea kazi kwa vitalu vya uzalishaji miche binafsi kwa vikundi kumi na saba kutoka wilaya Kaskazin B, Maharibi A na B na Naibu waziri Wizara Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe Lulu Msham Abdalla huko Maruhubi katika ofisi za Idara ya misitu na maliasili Zisizorejesheka. Amesema Wizara kupitia Idara ya Misitu INA lengo la kuhakikisha miche inapatikana kwa wananchi wote ili kuhifadhi na kulinda mali asili, mazingira na mali zisizorejesheka. Mhe, Lulu amesema kuwa mpango huo utasaidia kuweka hewa safi na afya kwa jamii ili kukuza uchumi katika nchi. Nao wazalishaji wa miche ya matunda na misitu wameiomba Idara ya misitu kuendeleza utaratibu wa utoaji wa vifaa na kupatiwa elimu zaidi ya uzalishaji wa miche. Jumla ya shilingi milioni nne (4,000,000) zimetumika kwa ajili ya kununulia vifaa kwa wazalishaji wa miche kwa msimu wa kilimo 2017/18