TAASISI YA OCEANOGRAPHY YAKABIZI VIFAA VYA UVUVI-August 2017

Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya OCEANOGRAPHY Ndugu Lian ZhangFei kutoka nchini china amemkabidhi vifaa vya uvuvi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Ndugu Maryam Juma Abdullah. Makabidhiano ya vifaa hivyo yametokana baada ya utoaji wa mafunzo ya ufugaji wa mazao ya baharini yaliyotolewa kwa muda wa wiki tatu, kwa wafugaji wa samaki, kaa na majongoo yaliyowashirikisha wafugaji 30 kutoka Unguja na Pemba.