ZIARA YA WAKULIMA WA KILIMO CHA MPUNGA WANAOTUMIA KILIMO SHADIDI-August 2017

Serikali imekuwa na juhudi za kulikuza zao la mpunga nchini kwa kupitia mradi wa kuongeza uzalishaji na tija katika zao la mpunga Zanzibar( ERPP) kwa kutumia mbinu bora za uzalishaji wa Mpunga kwa njia ya kilimo shadidi. Hatua za utowaji wa elimu ya kilimo shadidi zimekuwa zikichukuliwa na wawezeshaji ikiwemo uchaguzi wa mbengu bora za mpunga kwa kuwashirikisha wakulima wa mabonde yote ya Mpunga katika uchaguzi wa mbegu inayofaa kulimwa ambayo itawaletea tija na mavuno mazuri. Akizumgumza katika ziara ya wakulimawa mpunga waliotembelea bonde la Mtwango na Mwera, afisa utafiti ndugu Bakari kombo Mohamed amesema, mbegu ya SUPER BC na SARO ndio mbegu bora ambazo wakulima wa mpunga wanatakiwa kuzitumiakwani utafiti umeonesha kuwa na sifa za kustahamili maradhi,ukame pamoja na kuwa na uzazi mkubwa. Pia utafiti umeonesha mavuno yake ni wastani ya tani 4 mpaka 5 kwa hekta ambayo kwa kutumia mbegu hizi wakulima wataweza kukidhi mahitaji ya chakula na biashara. Akitowa maelezo kwa wa wakulima hao muwezeshaji kutoka mradi wa (ERPP) ndugu Mohamed Faida Haji, amewaeleza wakulima hao kilimo cha mpunga cha shadidi kinalengo la kumkomboa mkulima kwa kumuelimisha mbinu bora za uzalishaji wa mpunga, ambazo huazia katika uchanguaji wa mbegu zenye ubora zinazomuwezesha mkulima kuvuna mavuno mengi. Hivyo wakulima wawe tayari kuitumia taaluma hiyo kwani bado kunahitajika ongezeko la uzalishaji wa mpunga nchini ambao litapunguza uangizaji wa mchele kutoka nje ya nchi. Ziara hiyo iliwashirikisha wakulima mia moja kutoka mabonde yote ya mpunga imeendeshwa na mradi wa kilimo shadidi (ERPP).