UZINDUZI WA UVUNAJI WA MPUNGA BONDE LA PANGENI-July 2017

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi ndugu Juma Ali Juma amesema kilimo cha mpunga kinahitaji utumiaji wa pembejeo za kutosha ambazo zitamuwezesha mkulima kupata faida Akizinduwa uvunaji wa mpunga wa kutegemea mvua katika bonde la pangeni lenye eka 50 ambalo lilipatiwa pembejeo na serekali na kupewa kila mkulima eka moja ikiwa ni mpango wa Serekali kwa kila Wilaya. Pia aliwapongeza wakulima hao kwa mavuno mazuri ambayo yameweza kuleta mabadiliko ya ongezeko la mavuno kutoka polo 5 kwa eka na kufikia polo 35 kwa eka moja ni faraja kwa wakulima na taifa kwa ujumla kwani tunaelekea kwenye mapinduzi ya kilimo Aidha, ndugu Juma aliwataka wakulima wa mpunga kuongeza uzalishaji kwani lengo la Serekali kwa wakulima nikuweze kukuza usalishaji kwa ajili ya chakula na biashara kwavile Serekali haitaweza kuwapatia ruzuku wakulima wote wa mpunga nchini. nae katibu wa bonde la mpunga la pangeni ndugu juma faidhi aliishukuru wizara ya Kilimo Maliasili na Mifugo na Uvuvi kwa jitihada zake za kuwapatia wataalamu ambao wameshirikiana hadi kufikia mafanikio mazuri ya uzalishaji wa mpunga.