UANGAMIZAJI WA KIMA WAHARIBIFU KATIKA KISIWA CHA TUMBATU-February 2017

Tumbatu ni kisiwa ambacho kipo katika mkoa wa kaskazini A Unguja, Takribani mda mrefu kisiwa hichi kilikumbwa na usumbufu wa mazao kutokana na kushamiri kwa wanyama aina ya kima. Akiazimisha siku ya usasi Kitaifa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Hamad Rashid Mohamed akishirikiana na Kikosi kazi cha Usasi wa kitaifa kwa lengo la kuangamiza wanyama ambao wamekithiri katika uharibifu wa mazao ya wakulima katika kisiwa cha Tumbatu. Akiongoza kikosi kazi hicho na kuzindua usasi wa wanyama waharibifu wa mazao ya wakulima huko Tumbatu, Waziri wa Kilimo, Maliasili Mifugo na Uvuvi amewataka wananchi kuzidisha kasi ya kuzalisha chakula ili kuondokana na umasikini kwani kilio chao cha muda mrefu juu ya uharibifu wa mazao yao kwa kima yamefikia ukingoni. Akitoa shukurani zake kiongozi wa uperesheni wa usasi wa kitaifa kwa niaba ya wasasi wenzake amewataka wakulima na wananchi wa tumbatu kushirikiana ili zoezi hilo liweze kufanikiwa kwa salama. Nae sheha wa shehia ya tumbatu kwa niaba ya wananchi wa tumbatu amefarijika sana kuona ahadi ya Waziri juu ya kilio chao cha muda mrefu kimepatiwa ufumbuzi na kuwa na matumaini kwani wakulima na mazao yao kwa sasa yatakuwa salama. Zoezi hilo la uangamizaji wa wanyama waharibifu huko tumbatu litachukua siku tatu na linategemea kuangamiza kima wote wanaoharibu mazao.